Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Ali Reza A’rafi, katika hafla ya pamoja ya kuanza mwaka mpya wa masomo wa hawzah za wanawake kote nchini Iran, na Jamiatul-Zahra (s.a.), iliyopewa kaulimbiu ya “Ahadi ya Kitaaluma kwa Imam Aliyefariki Shahidi”, ambayo ilifanyika jana Jumamosi, tarehe 4 Mehr 1405 H.S, kwa kuhudhuriwa na wakurugenzi, walimu na baadhi ya viongozi, katika ukumbi wa Ayatullah Shar’i (ra) wa Kituo cha Uongozi wa hawzah za wanawake, alitoa pongezi kwa kuanza mwaka mpya wa masomo, akatoa shukrani na pongezi kwa juhudi za wote wanaoshiriki katika kukuza na kuinua taasisi hii ya kielimu, kidini na kimalezi, na akafafanua kuhusu nafasi, utambulisho, majukumu na dira ya hawzah za wanawake.
Pongezi kwa nafasi ya wanawake wa hawzah katika matukio ya hivi karibuni
Mkuu wa Hawzah nchini Iran, huku akiwapongeza wananchi, wapendwa, familia, wanafunzi wa hawzah, walimu, watumishi wa hawzah za wanawake pamoja na wakurugenzi wa mikoa, alisema: Tunapaswa kuwapongeza na kuwashukuru wote wanaofanya juhudi kwa ajili ya kukuza na kuinua taasisi hii adhimu na yenye heshima ya hawzah za wanawake nchini Iran na duniani. Hasa kutokana na nafasi ya kipekee sana, yenye kung’aa na isiyokuwa na mfano ambayo dada zetu watukufu waliitekeleza katika matukio ya hivi karibuni na katika vita vya tatu, tunapaswa kutoa pongezi na shukrani maalumu.
Bibi Fatimah Zahra (s.a.), mwendelezo wa wahyi na utume
Mkuu wa hawzah nchini Iran, alisema: Huzuni ya Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa ima kutokana na kukatika kwa wahyi, au kutokana na hofu juu ya mwendelezo wa utume na uongofu wa jamii, hizi ndizo huzuni mbili kuu za Mtume, na aya hizi, kwa kuzingatia uwezekano wa kushuka kwake tena, zinajibu huzuni hizo zote mbili.
Mwenyezi Mungu anasema: Usihuzunike kwa sababu ya kukatika kwa wahyi; wewe una nafasi ya juu, na pia anasema: Usihuzunike kuhusu mwendelezo wa utume; wewe unaye Fatimah. Usihuzunike kwa kukatika kwa wahyi, wala usihuzunike kwa kukosekana kwa mwendelezo; yote haya yanatibiwa kwa kuwepo Fatimah.
Ayatullah A’rafi alisisitiza: Mwenyezi Mungu alimjaalia Mtume (s.a.w.w.) Kawthar hii yenye kung’aa na jua hili lenye kutoa mwanga, ili awe na uhusiano na ulimwengu wa ghaibu na wakati huo huo aendelee kuangaza ulimwengu wa vitu vinavyoonekana na mustakabali wa historia.
Mwenyekiti wa Baraza la Sera la hawzah za wanawake alimchukulia BibiFatimah Zahra (s.a.) kuwa ni kiunganishi na udhihirisho wa nuru ya Mwenyezi Mungu, na kusema: Kiunganishi hiki huifikisha nuru ya Mwenyezi Mungu na mvuto wa mbinguni kwa wanadamu wote duniani; ni mwanamke mkubwa mwenye Wilaya ya Kimungu, Wilaya ya Kimaumbile ya Kimungu, pamoja na daraja hizo za kiroho na kiirfani ambazo zilikusanyika ndani yake.
Historia ya uwepo wa wanawake katika elimu na maarifa ya Kiislamu
Mkuu wa Hawzah nchini Iran, akiashiria historia ya uwepo wa wanawake katika uwanja wa elimu na maarifa ya Kiislamu, alisema: Hawzah za wanawake ni taasisi mpya, lakini wanawake wakubwa katika historia wamekuwa na uwepo katika shule ya elimu na maarifa ya Uislamu na maarifa ya Ahlul-Bayt (a.s.), na wametekeleza majukumu makubwa.
Kuanzia Bibi Khadijah (s.a.), Bibi Fatimah Zahra (s.a.), Bini Zaynab (s.a.) na wanawake wengine mashuhuri kama hao, hadi katika vipindi mbalimbali vya historia, kuna mnyororo mmoja wa kihistoria wenye baraka nyingi.
Ayatullah A’rafi, akirejelea vitabu vilivyoandikwa kuhusu wanawake Maswahaba wa Mtume (s.a.w.w.), alisema: Katika baadhi ya vyanzo, wametajwa zaidi ya wanawake 1,000 miongoni mwa Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) wa zama zake; hali ambayo idadi hiyo ilikuwepo katika zama ambazo mwanamke hakupewa nafasi yoyote katika jamii. Jambo hili linaonesha kwamba kuanzia mwanzo, suala la kumpa mwanamke nafasi na kumuwezesha kushiriki kikamilifu katika nyanja mbalimbali lilizingatiwa katika zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.).
Nafasi ya wanawake katika silsila ya wapokezi na wanazuoni wa hadithi
Mkuu wa Hawzah, akirejelea uwepo wa mamia ya wanawake wapokezi katika mnyororo wa wapokezi wa hadithi na maarifa ya Kiislamu, alisema: Katika mnyororo wa wapokezi wetu pia, kuna mamia ya wanawake wapokezi waliokuwepo katika mnyororo wa wapokezi na wanazuoni wa hadithi.
Alirejelea kitabu “Tanqih al-Maqal” cha marehemu Mamqani, na kusema: Miongoni mwa kazi ambazo zimekusanya suala hili kwa kiwango kizuri ni kitabu “Tanqih al-Maqal” cha marehemu Ma'mqani. Kitabu hiki ni miongoni mwa kazi muhimu katika elimu yetu ya Rijal, na ikiwa mtu atasoma utangulizi wake, atafahamu kazi kubwa na pana ambayo marehemu Ma'mqani aliifanya.
Ayatullah A’rafi aliendelea kusema: Marehemu Ma'mqani alianzisha mambo mawili au matatu ya ajabu sana, ambayo moja wapo ni hii “Tanqih al-Maqal”. Jana usiku pia nilikuwa nikisoma baadhi ya tafiti zake, na zilinivutia sana; miongoni mwa mambo hayo ni simulizi ambazo yeye mwenyewe alizitaja wakati wa kuandika kitabu hiki, pamoja na baadhi ya karama alizohisi.
Akirejelea ukubwa wa kazi hii, aliongeza: Mmoja wa wanazuoni wa Misri aliikosoa kazi hii mahali fulani na kusema: Kazi kubwa kiasi hiki ni kazi ya kundi kubwa sana; inawezekanaje mtu mmoja kuifanya kazi kama hii Walipomwalika na kumwambia kwamba mwanazuoni aliyeifanya kazi hii huko Najaf bado yupo, na kwamba athari na alama zake zote bado zipo, jambo hilo lilimshangaza sana, kwa sababu ilionekana kuwa haiwezekani kwa mtu mmoja, ndani ya muda mfupi, kuandika makumi ya vitabu vya kina katika elimu ya Rijal.
Maoni yako